Miguna aondoka kabla kuhojiwaMiguna aondoka kabla kuhojiwa
Siku moja tu baada ya mkurugenzi wa mashtaka ya Umma nchin Kenya kumtaka aliyekuwa mshauri wa waziri mkuu Miguna Miguna kuandikisha taarifa kwa polisi kuhusu madai yake, Miguna amearifiwa kusafiri kuelekea nchini Canada. Duru zetu katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta zimearifu kuwa Miguna alisafiri Jumatatu usiku. Hata hivyo, sababu yake halisi ya kusafiri haijabainika ingawa wandani wake wanadai kuwa anakwenda Canada kukiuza kitabu alichozindua jumamosi Peeling Back The Mask katika mataifa ya magharibi. Jumatatu mkurugenzi wa mashtaka ya Umma Keriako Tobiko alimtaka kamishna wa Polisi kuanzisha uchunguzi dhidi ya Miguna kuhusu madai yake kuwa ODM ilihusika kwenye ghasia za baada ya uchaguzi mkuu uliopita. Hata hivyo, Miguna alisema kwamba kuambatana na sheria ya kuwalinda mashahidi hapaswi kufichua anayoyajua kuhusu kupangwa kwa machafuko hayo.

Posted on 00:34. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for Miguna aondoka kabla kuhojiwa

Leave comment

.

Popular Posts

.

2012 Tz Celebs. All Rights Reserved.