EXCLUSIVE: Prezzo aachia ngoma ya diss kwa Jaguar (Download)

Beef la Prezzo na Jaguar ndio kama limeanza. Unakumbuka Jaguar alisema hana tatizo na Prezzo kwenda Big Brother kwakuwa amepata kitu kinachomfaa kufanya na sio muziki! Naye Prezzo akiwa tayari BBA aliwahi kusema kuwa hajawahi kuusikia wimbo wa Jaguar Kigeugeu! Basi mambo ndo yameanza upya kwakuwa Prezzo ameachia track ya kumdiss Jaguar. Katika wimbo huo wenye dakika 3:50 uitwao The Greatest, Prezzo amemshirikisha Plan B ambamo anajisifia kuwa hakuna mwingine kama yeye. Katika wimbo huo Prezzo anajinadi kwa kujifananisha na Mohamed Ali na kwamba Jaguar anamuonea wivu kwa mafaniko aliyonayo huku akimuita fala na mshamba. Kuna mstari anasema “ I am new school like Beats By Dre while you are (Jaguar)old school kama chopping screw” Mstari mwingine anasema “Mi kwenda down homeboy sahau, Keep my name at your mouth coz unajidharau, Hauwezani nami mshikaji maji yamezidi unga, nashindwa mbona ukiniona mdomo ushaufunga.” Usikilize na kudownload hapo chini. Yetu masikio kusubiri kama Jaguar atajibu!

Posted on 22:50. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for EXCLUSIVE: Prezzo aachia ngoma ya diss kwa Jaguar (Download)

Leave comment

.

Popular Posts

.

2012 Tz Celebs. All Rights Reserved.